August 17, 2018


Baada ya uongozi wa Yanga kuanza mchakato wa uchaguzi kwa ajili ya kuwapata viongozi walioachia ngazi, imeelezwa kuwa Kamati ya Uchaguzi imeamua kuibakisha nafasi ya Mwenyekiti wa klabu.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya hapo awali kuelezwa kuwa Yanga waliamua kuanza mchakato huo wakiwa na lengo la kumpata pia mbadala wa Mwenyekiti huyo lakini wameamua kugeuza gia angani na badala yake haitotumika kwenye uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ndani ya klabu hiyo, Bakili Makele, amesema bado wanamtambua Yusuph Manji kama Mwenyekiti wao hivyo kutakuwa na nafasi ya kumsaka Makamu na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Utendaji pekee.

Licha ya Manji kutuma barua ya kuomba kujizulu nafasi yake akiomba apumzike kutokana na kubanwa na mambo kadhaa, klabu hiyo ilipinga barua hiyo kupitia mkutano mkuu uliofanyika jijini Dar es Salaam Juni 10 2018.

Makele amesema Yanga bado inajua kuwa Mwenyekiti wake ni Manji hivyo nafasi yake ikiendelea kuwepo kama kawaida.


5 COMMENTS:

  1. Fikra finyu mawazo mgando mtu ashajiweka pembeni aachiwe mwingine alete fikra mbadala kauli mbiu sasa kwa wanayanga wote Yanga bila Manji inawezekana

    ReplyDelete
  2. FREDBALILE, @Kipindi cha uchaguzi ni kwa ajili ya nafasi zooote, wasiwafichie watu nafasi!

    ReplyDelete
  3. kweli mtu akikuita yanga kwangu naona ni bonge la tusi...hivi kweli ni akili mtu alishawatumia barua ya kujiuzulu mpaka leo bado mna mng'ang'ania...ina maana hakuna watu wenye akili zao ambao wanaweza kuiongoza yanga????ki ualisia manji yanga hawezi rudi kwa maana kwa sasa haina mchango kwake, kwanza sasa hivi mambo yake hayapo sawa alikuwa anamiliki kampuni ya usafirishaji mambo yamekwenda mrama kapunguza stuff wote kifupi sasa hivi siyo manji wa zamani...kwanini msiende kumwomba Mengi akaja akawapa uhai...YANGA NZIMA MWENYE AKILI NI MZEE AKILI MALI PEKEE

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jamani sasa mmeamua kutuona wana Yanga wote hatufikiri vizuri ila mzee Akilimali peke yake? Hiyo sawa kweli?

      Delete
  4. Mmhh kumbe yanga hakuna mwenye akili ya kuongoza klab zaidi ya Manji....aibuuuu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic