September 10, 2018


Na George Mganga

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawakumbusha Wanachama wake kwamba hairuhusiwi timu ya Mpira wa Miguu kutoka nje ya nchi kucheza mechi ya kirafiki au kushiriki mashindano hapa nchini bila ya kibali kutoka TFF na pia kukamilisha taratibu zilizowekwa na FIFA.

TFF imesema kuwa ni vema kwa vilabu hivyo kufanya taratibu hizo ambazo zimewekwa kwa mujibu wa shirikisho pamoja na FIFA.


Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashindano, Salum Madadi, amesema wamefikia hatua ya kuzikumbusha timu ikiwa ni baada ya Simba kuwaalika AFC Leopards ya Kenya kuja nchini kucheza bila kufuata taratibu maalum.

Madadi amesema suala hilo la Simba limewashtua wengi na kufikia maamuzi ya kuwaamua kulikumbushia tena ili kuweka mambo sawa.

"Tumeamua kulikumbushia hili kulingana na hivi karibuni kuna timu mbili kutoka nje ya Tanzania zilikuja kucheza na Simba pamoja na Biashara United bila kufuata taratibu rasmi ambazo zimewekwa kwa mujibu wa TFF na FIFA" alisema.


4 COMMENTS:

  1. Sina uhakika lakini kule ulaya timu zilizo kwenye jumuiya ya ulaya sizani kama kuna nasharti na vipingamizi vya kiasi hicho. Kenya,Uganda,Tanzania, Rwanda.Burundi mpaka Sudani kusini ni miongoni mwa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki hata kuwaita wachezaji wa nchi hizo ni wa kigeni sidhani kama ni sahihi kwa afya na ustawi na uhusiano wa kimichezo katika eneo letu.

    ReplyDelete
  2. Kupenda ukubwa tu.Wanazisaidiaje timu?Kazi kulaumu tu?

    ReplyDelete
  3. Bifu za kipumbavu hasa kwa Simba.TFF inatumia nguvu kubwa kulamisha migogoro na vilabu badala ya kuvisaidia yaani hovyo kabisa.

    ReplyDelete
  4. Kwa upande wangu nafikiri ni sahihi. TFF haijalalamika bali imevikumbusha vilabu kufuata taratibu zilizowekwa. Hata ulaya timu kutoka nchi moja kwenda kucheza sehem nyingine.. Lazima shirikisho la soka kwa nchi husiska litambue kama kuna mechi itachezwa. Hata hivyo ni kanuni za FIFA na wala sio TFF. TFF wamefanya kukumbushia tu ili Simba na timu nyingine zisiingie kwenye matatzo. Maana kuna faini kwa timu mwenyeji.@Anonymous

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic