September 10, 2018


Na George Mganga

Mwanachama mkongwe wa Simba, Mwina Kaduguda, leo amejitokeza kuchukua fomu kunako makao makuu ya klabu hiyo.

Kaduguda amefikia maamuzi hayo baada ya baadhi ya wanachama kuchanga kiasi cha laki tatu kisha kumlipia kwa ajili ya kuwania nafasi ya Mjumbe wa Bodi ya Udhamini.

Mwanachama huyo ambaye aliwahi kuwa kiongozi ndani ya klabu hiyo, ameonekana kupewa imani na wadau wengi wa Simba na kumtaka afanye maamuzi hayo haraka.

Nguvu za wanachama hao zimesaidia Kaduguda kutochelewa kuchukua fomu hiyo ambapo leo ndiyo siku ya mwisho kwa walio na sifa kuchukua fomu hizo.

Klabu ya Simba itafanya uchaguzi wake mkuu Novemba 3 2018 kwa ajili ya kuwapata viongozi wapya amba watakuwa na mamlaka ya kuiongoza Simba kwa miaka minne ijayo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic