September 19, 2018


Kiungo mshambuliaji kipenzi cha Wanayanga, Ibrahim Ajibu amewaambia mashabiki wa timu hiyo waondoe hofu yapo mambo mengi yanakuja kuelekea mchezo dhidi ya watani wao wa jadi, Simba.

Kauli hiyo aliitoa siku chache baada ya kuonyesha kiwango kikubwa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Stand United huku yeye akifunga bao moja na kutengeneza mabao matatu kwa Mrisho Ngassa, Andrew Vincent na Deus Kaseke.

Mshambuliaji huyo hivi karibuni alibezwa kutokana na kiwango kidogo alichokuwa anakionyesha kwenye michezo kadhaa.

Ajibu alisema shukrani kubwa ziende kwa kocha wake Mwinyi Zahera ambaye ndiye amembadilisha kwa kiwango.

“Sikuwa fiti kwenye michezo iliyopita na huo ndiyo ukweli, lakini hivi sasa nipo fiti baada ya kufanyia kazi maelekezo na mbinu ambazo kocha wangu ananipa.

“Mara kadhaa kocha amekuwa akinisisitiza umakini nikiwa uwanjani kwa kutimiza majukumu ambayo amekuwa akinipa, hivyo basi nashukuru hilo nimelifanyia kazi ndiyo sababu ya mimi leo kuonekana nimebadilika.

“Niwaahidi Wanayanga kuwa, yapo mengi yanakuja Yanga na kikubwa tunahitaji sapoti yao kwa kujitokeza uwanjani kwa ajili ya kutuunga mkono ili kuhakikisha tunapata matokeo mazuri ya ushindi hilo jambo la muhimu, tunaamini kuwa tutafanya vizuri kwenye michezo yote ijayo,” alisema Ajibu.

Yanga wana michezo mitatu ya hivi karibuni dhidi ya Coastal, Singida na JKT Tanzania kabla hawajavaana na Simba, Septemba 30.

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic