Baada ya kamati ya Tuzo ya Ligi Kuu Bara kumtaja mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere ameweka wazi kuwa kupata tuzo ya Mchezaji Bora wa mwezi Agosti ni faraja kwake kutokana na watu kuiona kazi yake.
Kagere alipata tuzo hiyo baada ya kuwazidi wachezaji aliokuwa anashindanishwa nao ambao ni Omary Mponda wa Kagera Sugar mwenye mabao 2 na Joseph Mahundi wa Azam FC mwenye mabao 2, huku Kagere akiwa na mabao 3 baada ya kucheza mechi mbili.
Kagere alisema kuwa ni jambo la faraja hasa kwa kazi yake kuweza kuonekana na watu kuithamini hivyo anaamini huo kwake ni mwanzo mzuri na hakuwa na muda wa kumfuatilia Makambo wakati Yanga ilipocheza na Stand United.
“Ninawashukuru sana ambao wameniteua na kunipa tuzo hiyo ya mchezaji wa mwezi nasema Asante, ila mafanikio haya ni kwa ajili ya timu yangu na mashabiki ambao wapo pamoja nasi bega kwa bega.
“Kila baada ya kumaliza mchezo mmoja natambua kuwa kuna mwingine unakuja hivyo napenda sana kuwashukuru, kuhusu kutumia muda wangu kutazama mchezo wa Yanga sijafanya hivyo kwa kuwa nilikuwa nafuatilia ligi ya Ulaya” alisema Kagere aliyekipiga Gor Mahia ya Kenya kabla ya kutua Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment