Mgunda amekubaliana na matokeo hayo ambayo walikuwa hawayatarajii lakini ameona si kesi na badala yake atakifanyia marekebisho kikosi.
Kocha huyo ameeleza kuwa kikosi chake kimeonesha mapungufu kadhaa ambayo watayarekebisha ili kuja upya tayari kumalizana na Yanga katika mechi ijayo.
Mgunda amesema nguvu zake zote zitaelekezwa kukiandaa kikosi kuja kivingine ili kupambana na Yana vizuri na ikiwezekana kuchukua alama zao tatu.
Katika mchezo huo, mchezaji Ali Kiba aliyesajiliwa kwa mwaka mmoja hakuweza kucheza japo alihudhuria uwanjani kuwapa morali wachezaji wenzake.
0 COMMENTS:
Post a Comment