September 11, 2018


Staa wa Afro Pop ndani na nje ya Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz,  ameamua kuweka wazi maisha yake ya mahusiano na kusema kuwa kwa sasa hana mahusiano na mwanamke yeyote.

Diamond ambaye amekuwa akisemwa kwa kuwa na mahusiano na wanawake wengi tofauti, ameandika katika ukurasa wake wa Snapchat na kusema kuwa kwa sasa yeye ni ‘single boy’.

Ukiachana na kuwa amekuwa akitamaniwa na wanawake wengi, inawezekana ikawa ni moja ya njia aliyoamua kuitumia ili kuwonyesha baadhi ya wanawake kuwa kwa sasa yuko ‘free’ na anatafuta mwanamke wa kuwa naye katika mahusiano.


Diamond ni mmoja wa wasanii wanaoongoza kwa kuwa na msululu wa wasichana mbali ya wale ambao amekuwa akiwakana. Kuna wanawake wengi ambao walikuwa wakijulikana kwa uwazi kutokana na kuyaanika mahusiano yake na wao.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic