RAMOS AZIDI KUMSALITI RONALDO, AIBUKIA KWA MODRIC
Beki wa Real Madrid Sergio Ramos amesema kuwa Luka Modric ndiye mchezaji mwenye sifa za kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Kiume wa FIFA mwaka 2018 dhidi ya Ronaldo na Mohammed Salah.
Ramos ameeleza kuwa Modric ni moja ya wachezaji wachache anaowakubali katika kikosi cha Los Blancos.
Uchaguzi wa Ramos kwa Modric umekuja kutokana na mchango aliouonesha mchezaji huyo kwenye michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Urusi mwaka huu.
Ramos anaamini Modric anastahili kutokana na juhudu zake za uchezeshaji na upikaji wa mipira kama kiungo.








0 COMMENTS:
Post a Comment