TAIFA!!! HATA KAUNDA MBONA POA TU
Uongozi wa klabu ya Simba kupitia kwa Ofisa Habari wake Haji Manara, ameweka msisitizo kuhusiana na ratiba ya ligi inayoonesha mechi 7 za Yanga kuchezwa Uwanja wa Taifa.
Manara ameeleza kuwa wao kama Simba wala hawana hofu huku akijigamba hata kama watacheza michezo yote ya ligi kwenye Uwanja wa Kaunda wala haina tatizo.
Ofisa huyo ameibuka na kuwataka Yanga endapo ratiba hiyo ikija kupangwa upande wao kama Simba wasije wakaibuka na kuanza kuitupia lawama TFF kuwa inawapendelea.
Manara amekumbushia kuwa wakati ratiba ya ligi haijaanza walilalamika kuwa shirikisho hilo linawapendelea baada ya kupangiwa mechi kadhaa za ugenini ambapo Simba alikuwa anaanzia nyumbani Dar es Salaam.
Lakini baada ya kuja tena kufanyiwa mabadiliko, Manara amesema wao wanaheshimu maamuzi ya bodi ya ligi na akisema hawana kinyongo hata kama mechi zote wakichezea pale kwenye uwanja wao wa Kaunda haiwezi kuwa tabu.
0 COMMENTS:
Post a Comment