HERRERA, MOURINHO, POGBA, DE JONG: TETESI KUBWA ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE
Manchester United na Real Madrid wana mipango ya kumsaini kiungo wa kati wa Ajax Mholanzi mwenye miaka 21, Frenkie de Jong, anayewekewa thamani ya pauni milioni 72. (De Telegraaf - in Dutch)
Kiungo wa kati wa Uhispania Ander Herrera, 29, angetaka kubaki huko Old Trufford licha ya Barcelona kumzea mate. (ESPN)
Arsenal wanamwinda mchezaji wa Rennes raia wa Senegal mwenye miaka 20 Ismaila Sarr, ambaye pia anatazamwa na Inter Milan.(Mirror)
NewCastle watafanya mkutano na meneja Rafael Benitez kuhusu bajeti ya mwezi Januari kujaribu kumwezesha Mhispania huyo kusalia kwenye klabu baada ya mwisho wa msimu. (Telegraph)
Paris-St Germain wanammezea mate beki wa Juventus mwenye miaka 27 Mbrazil Alex Sandro, ambaye awali amehusishwa na Manchester United. (Le10 Sport - in French)
West Ham wako kwenye hatari ya kumpoteza mlinzi wa miaka 19 raia wa Ireland Declan Rice baada ya kukataa nyongeza ya mshahara wa pauni 12,000 kwa wiki. (Mail)
Arsenal, Manchester United, Liverpool, Chelsea na Newcastle ni kati ya vilabu 18 ambavyo vimewatuma maajenti kumtazama kipa wa Benfica Mjerumani Odisseas Vlachodimos, 24. (Record - in Portuguese)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alimlaumu kiungo wa kati Paul Pogba, 25, kwa bao lilifungwa na Wolves huko Old Trafford siku ya Jumamosi. (Sun)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment