September 25, 2018


Na George Mganga

Kuelekea mechi ya watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Simba, imeelezwa Mwamuzi atakayechezesha pambano hilo atakuwa ni Mwanamama Florentina Zabron kutoka Dodoma.

Mwanamama Florentina atachezesha pambano hilo ambalo huvuta hisia za mashabiki wa timu zote mbili pamoja na wadau wake Septemba 30 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Tayari Simba na Yanga zimeshaondoka jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza mawindo ya mechi hiyo kubwa Jumapili ya wiki hii.

Timu zote mbili zimeanza kambi baada ya kusogezewa mbele mechi zao ambazo walipaswa kuzipiga kabla hawajakutana kuelekea mechi baina yao.

Awali ratiba ilionesha Simba walipaswa kucheza na Biashara United Septemba 27 na Yanga dhidi ya JKT Tanzania Septemba 26 lakini ratiba hiyo ilibatilishwa na sasa itapangwa upya.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic