KAGERE ATUPIA MOJA KAMBANI KUELEKEA AFCON RWANDA IKILALA 2-1 VS IVORY COAST
Timu ya Taifa ya Rwanda 'Amavubi' mimepoteza mchezo wa kuwania kucheza fainali za AFCON 2019 kwa mabao 2-1 dhidi ya Ivory Coast.
Mabao ya Ivory Coast yamewekwa kimiani na wachezaji Kodija na Gradel huku bao pelee la Rwanda likifungwa na straika hatari wa Simba, Meddie Kagere.
Amavubi wamekipiga na Ivory Coast wakiwa na wachezaji wawili wanaokipiga ndani ya klabu ya Simba ambao ni Haruna Niyonzima na Kagere ambaye amefunga.
Baada ya Niyonzima na Kagere kumaliza kibarua hicho, wachezaji hao wanatarajiwa kuanza safari kesho au keshokutwa kuanza kurejea Dar es Salaam kujiunga na klabu yao kwa maandalizi ya mechi zijazo.








Kagere sio wa mchezo mchezo nashngaa watu kumpambanisha na Makambo.
ReplyDeleteKagere,Makambo sio saizi yake. Wakati Makambo akishindwa kupachika bao katika mechi ya Ndondo kati ya Yanga na African Lyon Kagere anaifungia timu yake ya Taifa dhidi ya miongoni mwa timu bora ya taifa barani Africa.
Hapo ndyo tutakapoanza tena kumsubiri Niyonzima hadi mzunguko wa kwanza unaisha. Hakuna kinachonikera kama kuchelewa kuripoti kambini.
ReplyDelete