September 13, 2018


Kamati ya uchaguzi ya klabu ya Simba imetoa onyo kwa wagombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kuepuka kuenguliwa haraka.

Simba itafanya uchaguzi wake Novemba 3 2018 ili kuwapata viongozi wake wapya watakaochukua nafasi za waliomaliza muda wake ikiwa katika mfumo mpya na wa kisasa kiuendeshwaji.

Kamati hiyo imekuja na onyo kwa kuwakumbusha wagombea wote kufuata sheria na kanuni za kampeni ili kuepuka kukatwa kwa maana wasubirie mpaka muda maalum utakapowadia.

Kamati hiyo imewakumbushia wagombea hao kuzingatia masharti ya kampeni ili kukwepa msala wa kukosa sifa za kuhusika kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe tajwa hapo juu.

Tayari baadhi ya wagombea wameshaanza kurejesha fomu zao mara baada ya zoezi la kuchukua kufungwa tayari kusubiri siku maalum za kuanza kampeni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic