September 13, 2018


Na George Mganga

Baada ya zoezi la kurejesha fomu za wagombea nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya klabu ya Simba, Mwanachama Mtemi Ramadhani ambaye ni miongoni waliochukua fomu ya kugombea amesema atarejesha ndani ya muda wowote kuanzia leo.

Ramadhani ambaye anawania nafasi ya Uenyekiti ndani ya klabu hiyo, ameeleza kuwa kwa sasa hawezi kusema lolote kwa maana muda wa kupiga kampeni bado haujafika.

Kwa mujibu wa Radio One, Mwanachama huyo amesema hayo kwa hofu ya kuenguliwa ili kufuata sheria na taratibu za kampeni ambapo mpaka muda maalum ufike ndiyo ataruhusiwa kunadi sera zake.

Katika nafasi ya Uenyekiti, Ramadhani yupo na Swedy Mkwabi wakiwa wawili pekee wanaowania nafasi hiyo wakati wajumbe wakiwa wengi zaidi.

Simba itafanya uchaguzi wake Novemba 3 2018 ili kupata watawala wengine wapya baada ya hawa waliopo madarakani muda wao kumalizika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic