September 11, 2018


Licha ya watani zao wa jadi Simba kuwapiga majungu baada ya kuanzisha harambee ya kuomba michango ya fedha ili kuipa nguvu klabu, imeelezwa fedha hizo zimeanza kuweka mambo sawa katika klabu ya Yanga.

Taarifa zilizo ndani ya uongozi wa Yanga zinasema kuwa mabosi wa timu hiyo wamefurahia mchango ambao unazidi kutolewa na wanachama wake ambao umekuwa ikiipa sapoti timu yao mpaka sasa.

Yanga imekusanya kiasi cha shilingi za kitanzania zaidi ya milioni 30 kwa mwezi uliopita ambazo zimekuwa chachu ya mafanikio tangu kuanzishwa kwa kampeni hiyo maalum.

Unaambiwa fedha za wanachama wa klabu hiyo wenye mapenzi ya dhati na timu imesaidia pia harakati za kuisaifirisha timu kuelekea Rwanda kwa ajili ya kukipiga na Rayon Sports kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Kutokana na kuleta manufaa ndani ya klabu, fedha hizo sasa zinawapa majibu watani zao wa jadi Simba waliokuwa wakikebehi namna walivyoanzisha mpango huo wa kuchngisha fedha.

3 COMMENTS:

  1. Kumbe bakuli bado ndilo wanalolitegemea yanga. Kwa safari limesaidi vipi kuhusu mishahara ya kila mwezi inayokadiriwa kwa mamilioni si tumesikia Manji anaitaka yanga mpya na kuahidi usajili mpya na huku wanadai kuwafunga midomo wanaowabeza kumbe hamna lolote na si hasha kesho ukasikia tena pesa za Manji zinafoka na kempu mpya Ujarumani na jamaa wanatamba mitaani kwa bakuli. Tuseme Manji anawadanganya au ni wao wenyewe tu.

    ReplyDelete
  2. Watachangishana mpakalini safari ndefu watu watachoka watanzania awanauvumilivu

    ReplyDelete
  3. Watachangishana mpakalini safari ndefu watu watachoka watanzania awanauvumilivu mlisema kanji amerejea sasa nimwendo wamabakuli akuna cha manji wala kanji

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic