September 11, 2018


Mshambuliaji mpya wa Simba aliyesajiliwa hivi karibuni, Marcel Kaheza, amesema kuwa lengo lake ni kuhakikisha anapambana kusaka namba ya kumuwezesha kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza.

Kaheza ambaye alisajiliwa na wekundu hao wa Msimbazi akitokea Majimaji FC baada ya timu hiyo kushuka daraja, ameahidi kupigana kufa na kupona ili kumshawishi kocha wake, Mbelgiji, Patrick Aussems, aweze kumpa namba.

Mshambuliaji huyo amepata jeuri hiyo baada ya kutupia bao katika mchezo wa juzi dhidi ya AFC Leopards ya Kenya uliokuwa wa kirafiki ambapo Simba ilishinda kwa mabao 4-2.

Kinda huyo anaamini atatumia vema nafasi anazozipata akiwa na mpira ndani ya uwanja kuhakikisha hapotezi nafasi hizo.

Wakati Kaheza akiahidi kutaka namba kikosi cha kwanza, Simba hivi sasa wapo wenye maandalizi ya mechi zijazo za ligi ikiwa ni baada ya kusimama kwa muda ili kupisha mechi za kimataifa.

1 COMMENTS:

  1. Vijana wetu wanavipaji lakini waoga mno wanakosa ujasiri hakuna kingine chochote kinachowasumbua. Bila ya ujasiri kamwe huwezi kuutwaa ushujaa. Kitu gani kinachompa kigugumizi kaheza kuonesha uwezo wake pale Simba au kelele za mji zinamzingua? Kule majimaji alikuwa hashikiki kaja hapa mjini ni wa kawaida sana? Wakati yupo majimaji Kaheza alikuwa ana uwezo wa kufunga mechi ambazo Okwi au Boko hawezi.Ukimuangalia kaheza ni moja kati ya vijana wenye mwili ambao anaweza kufanya anachotaka katika mpira.Mbape licha ya udogo wake umbo na umri na kimo kamwe hafikirii atapata vipi namba mbele ya OliverGeroud au Edison Cavan,anachokijua yeye ni kufanya kile anachotakiwa kufanya. Kaheza alitakiwa hivi sasa sio kufikiria kupata namba Simba alitakiwa ajiulize kwanini Shabani chilunda kaitwa timu ya Taifa na yeye hata kufikiriwa hafikiriwi kuitwa kwanini wakati yeye ni miongoni mwa wafungaji mahiri? Kaheza, Salamba ni wakati muafaka wa kupigania namba timu ya Taifa na hakuna lisilowezekana wakiamua. Hayo masuala ya kusema sijui nimepanga hivi au naanza kupigania namba ni dalili za mchecheto kwani mwanaume wa kweli wakwenda kumfumania mwizi anaemkazia mkewe huwa hatoi habari kwamba nakuja huko ni kuvunja dirisha au mlango kumkabili mwizi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic