KISA YANGA, KADUGUDA AITIKIA WITO HUU KUTOKA KWA WANASIMBA
Hii ni balaa, wanachama wa klabu ya Simba wametangaza kumchukulia fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti Mwina Kaduguda endapo hatofanya maamuzi mwenyewe.
Wanachama hao wameeleza kuwa na imani na Mwanacha huyo mkongwe aliyewahi kuwa kiongozi wa juu kunako klabu hiyo iliyo mitaa ya Msimbazi, Kariakoo, Dar es Salaam.
Kaduguda mwenyewe amefunguka kwa kusema kuwa amepata taarifa zao wakimtaka afanye maamuzi ya kuchukua fomu haraka na asipofanya hivyo watampelekea wenyewe.
Kaduguda amesema wanachama hao wamemtaka kufanya hivyo la sivyo watamchukulia kuwa yeye ni Yanga na kutokana na kauli hiyo imebidi aitie wito.
Uongozi wa Simba umewataka wanachama kujitokeza kwa wingi leo kunako makao makuu kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Novemba 3 2018.








0 COMMENTS:
Post a Comment