September 10, 2018


Zinedine Zidane amezidi kumpa tumbo joto kocha wa Manchester United Jose Mourinho baada ya kukiri kuwa atarejea kufundisha soka muda mfupi ujao.

Kwa wiki kadhaa sasa imekuwa ikielezwa kuwa Mourinho atatimuliwa na kwamba Zidane ndiye kocha mpya ajaye Manchester United.

Kupitia vyombo mbalimbali vya habari Ulaya, vimekuwa vikiripoti kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Zidane kuchukua nafasi ya Mourinho pale United kutokana na kuwa na mwenendo mbaya na timu hiyo.

Uwepo wa taarifa hizo umezidi kushika kasi zaidi na hii ni kutokana na United kushindwa kufanya vizuri kwa siku za hivi karibuni, hivyo nafasi ya Mourinho kuendelea kusalia Old Trafford inatia shaka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic