September 15, 2018


Baada ya kuingoza Taifa Stars kwenda suluhu ya kutofungana na Uganda The Cranes katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza AFCON 2019, Kocha Emmanuel Amunike amekwea pipa kuelekea Hispania.

Amunike ameondoka nchini na shirika la ndege 'Qatar Airways' kuelekea nchini huko kwa mapumziko kabla ya kurejea tena Tanzania kwa kuanza maandalizi ya kuiandaa Stars kuelekea mechi dhidi ya Cape Verde.

Kocha huyo atawasili tena nchini kuanzia Septemba 22 tayari kwa kambi nyingine maalum ambayo itaanza Oktoba 1 kuelekea mechi hiyo ya kufuzu AFCON.

Stars itacheza na Cape Verde Oktoba 10 kuendelea na harakati za kuwania tiketi za kucheza AFCON mwakani.

2 COMMENTS:

  1. ligi imeanza ulikuwa wakti wake mzuri wa kuangalia viwango vya wachezaji

    ReplyDelete
  2. KOCHA HANA MUDA WA KUANGALIA WACHEZAJI WANAOCHEZA LIGI? HIYO NI NAFASI NZURI KWA KOCHA ANAYEJALI KAZI KUWAANGALIA WACHEZAJI WALIOPO NCHINI. BADALA YAKE ANAKIMBILIA KUONA FAMILIA YAKE. SAWA MAANA YOTE TUNAMUUNGA MKONO SAWA MZEE

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic