September 10, 2018


Na George Mganga

Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Morocco, amesema kikosi kinatarajia kuingia tena kambini kuanzia tarehe za kuelekea mwisho wa mwezi kwa ajili ya kambi maalum dhidi ya Cape Verde.

Stars na Verde zitakutana zilizo kundi L zitakutana Oktoba 10 2018 ambapo Stars itakuwa ugenini.

Kwa mujibu wa Radio EFM, Morocco ameeleza kuwa kwa sasa wamewaachia wachezaji ili wakazitumikie klabu zao kabla hawajakutana tena kwa ajili ya kuwania tiketi ya kufuzu AFCON 2019.

Stars imetoka kucheza na Uganda na kuwafanikiwa kwenda suluhu tasa ya bila kufungana na kuifanya ifikishe alama mbili baada ya kwenda sare ya 1-1 na Lesotho jijini Dar es Salaam.

Kuelekea kambi hiyo, Morocco amezungumzia wachezaji wa Simba waliotemwa kama wanaweza wakarejeshwa kikosini kuwa ni mapema zaidi kwa sasa kufanya hivyo hivyo subira inahitajika.

Wachezaji hao waliondolewa kikosini na Kocha Mkuu, Emmanuel Amunike, kutokana na kuchelewa kuripoti kambini lakini baadaye aliwasamehe na kuahidi kuwaita tena siku za usoni endapo watamshawishi kwa viwango vyao.

"Ni mapema sana kulizungumzia hilo kwa sasa, nadhani kuwe na subira" amesema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic