September 1, 2018


Licha ya straika wa Simba, Meddie Kagere kufunga mabao matatu mpaka sasa kwenye Ligi Kuu, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji Patrick Aussems amesema anaona haitoshi hivyo anahitaji zaidi ya hayo.

Kagere kwa sasa ndiye kinara wa mabao Simba na Ligi Kuu Bara baada ya kufunga mabao matatu kwenye michezo miwili aliyocheza ambayo ni dhidi ya Prisons alitupia bao moja na Mbeya City mabao mawili.

Mbelgiji huyo ameliambia Championi Jumamosi kuwa, straika wake huyo anatakiwa kuongeza kasi zaidi ili afunge mabao mengi yatakayosaidia kuibeba timu hiyo na kutetea ubingwa wao wa ligi kuu.

“Siyo mbaya kwa namna ambavyo amekuwa akifanya japo kwangu naona bado haitoshi anatakiwa kufunga zaidi na zaidi kadiri ya timu itakavyoshuka dimbani lakini kutengeneza nafasi kwa wenzake kwa ajili ya kupata mabao.

“Yeye ni mmoja wa washambuliaji wazuri tulionao hapa na lazima aonyeshe makali yake kwa kufunga katika michezo yetu,” alisema Mbelgiji huyo.

1 COMMENTS:

  1. Anastahiki sifa kwasababu amejijenga kinidhamu lakini mkono mmoja haupigi kofi na jambo kubwa pia namna anashirikiana na namna vijana wanavomlisha mipira. Asante kocha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic