MKUSANYIKO WA HABARI KUBWA ZA SOKA KIMATAIFA
Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 25, alichunguzwa na maskauti wa Barcelona wakati wa mechi ya vilabu bingwa ya ushindi dhidi ya Young Boys. (Mundo Deportivo - in Spanish)
United inaongoza vilabu vya ligi ya Uingereza kurudisha tarehe ya mwisho ya uhamisho kuwa mwisho wa mwezi wa Agosti. (Mail)
Nyota wa Spurs Christian Eriksen, Toby Alderweireld na Danny Rose wanataka malipo yao kuongezwa ili kuwa sawa na yale ya Harry Kane ambaye analipwa kitita cha £200,000 kwa wiki. (Sun)
Mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud analengwa na klabu ya Besiktas. Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 31 hana kandarasi katika klabu ya Chelsea msimu ujao . (Goal - in Turkish)
Kiungo wa kati wa klabu ya Paris St-Germain na Ufaransa Adrien Rabiot, 23, yuko tayari kujiunga na Manchester City kwa uhamisho usiokuwa na malipo wakati kandarasi yake itakapokwisha mwisho wa msimu huu. (Metro)
Mkufunzi wa zamani wa Swansea Carlos Carvalhal anataka kupewa fursa nyengine katika kufunza katika ligi ya Uingereza.. (Times - subscription required)
Barcelona inajiandaa kuwasilisha ombi la kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United Ander Herrera, 29.
Mabingwa hao wa La Liga waliwasilisha ombi lao kwa raia huyo wa Uhipania , ambaye kandarasi yake katika klabu hiyo ya Old Trafford inakamilika msimu ujao wakati wa siku ya mwisho wa dirisha la uhamisho.. (Sun)
Winga wa Everton na England Theo Walcott, 29, anasema kuwa alikuwa amepoteza hamu yake kucheza soka alipoondoka Arsenal mnamo mwezi Januari.(mirror)
Kipa wa Arsenal na Ujerumani mwenye umri wa miaka 26 Bernd Leno, ambaye alisajiliwa na klabu hiyo kutoka klabu ya Ujerumani ya Bayer Leverkusen, anasema hafurahishwi kuwa mchezaji wa Akiba wa Czech mwenye umri wa miaka 36.(Evening Standard)
0 COMMENTS:
Post a Comment