MWAKINYO APOKEA MILIONI HIZI BUNGENI DODOMA LEO
Bondia Hassan Mwakinyo amepewa zawadi ya Tsh. Milioni 7.2 baada ya kuchangiwa Sh. 20,000 na kila mbunge alipotembelea Bunge jijini Dodoma leo kufuatia ushindi aliyoupata hivi karibuni.
Mwakinyo ambaye ni mzaliwa wa Tanga, alimtwanga Bondia Mwingereza Sam Egginton kwa TKO katika raundi ya pili pekee.
Kiasi hicho cha milioni 7.2 amekipokea leo baada ya kukabilishwa bungeni Dodoma kumpongeza kutokana na kile alichokifanya kwa kuiwakilisha Tanzania vema.
Ukaribisho wa bondia huyo Bungeni ulichagizwa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe baada ya kumpa pongezi kwa kumchapa Mwingereza huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment