September 24, 2018


Na George Mganga

Yawezeka ikawa pengo na pigo kwa Yanga ambapo mchezaji wake aliyekuja kwa kasi, Mkongomani, Heritier Makambo yupo kwenye hatihati ya kuikosa mechi ya watani wa ajdi dhidi ya Simba.

Makambo hakuwepo kwenye kikosi cha jana kilichocheza dhidi ya Singida United na kufanikiwa kuibuka na mabao 2-0 dhidi ya Singida United.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Yanga zinasema straika huyo alikuwa hayuko fiti licha ya kufanya mazoezi siku ya mwisho kuelekea mechi na Singida lakini jina lake likakosekana katika kikosi cha jana.

Katika mchezo huo, Zahera alimpa majukumu Amis Tambwe akichukua nafasi ya Makambo na kufanikiwa kutupia mabao mawili yakiwa ni ya ushindi dhidi ya Singida United.

Licha ya kuikosa Singida, inaelezwa pia hali ya mchezaji huyo si mbaya kiasi cha kwamba uwezekano wa kucheza dhidi ya Simba kwa asilimia kubwa, mechi ambayo itapigwa Septemba 30 2018.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic