September 24, 2018


Licha ya wachezaji watatu wa klabu ya Yanga kusamehewa baada ya kuomba msamaha kwa mmabosi wa timu hiyo, mpaka sasa haijajulikana kipa kinda Ramadhan Kabwili atarejea lini kikosini.

Yanga iliwasamehe Pius Buswita, Abdallah Shaibu na Said Makapua ambao waliondolewa kambini kwa utovu wa nidhamu kisha kukaa nje ya kambi kwa siku takribani tatu.

Wachezaji hao walisamehewa na Kocha Mkuu Mwinyi Zahera pamoja na mabosi wa klabu hiyo lakini mpaka sasa haijajulikana hatm ya Kabwili ambaye mpaka sasa hajarejeshwa kambini.

Kipa huyo ambaye ni zao la Serengeti Boys aliondolewa kwenye kikosi na Kocha Zahera kwa kuchelewa kuripoti kambini, jambo ambalo lilimkasilisha kinoma kocha huyo.

Tayari Makapu, Ninja na Buswita wameongeza nguvu kuelekea mechi dhidi ya watani zao wa jadi Simba itakayopigwa Septemba 30 2018.

2 COMMENTS:

  1. Wamwache atafute timu dirisha dogo. Hii ni hazina ya Taifa wanaiharibu .Kindoki hana uwezo kumshinda Kabwili

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ktk kila timu ukiwa ni kipa no 3 unacheza mara chache sana jiulize katika timu za azam na samba pia nani kachezesha hata kipa na mbili kwenye hii ligi!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic