Mshambuliaji wa Simba, Adam Salamba amesema amekuwa akivutiwa zaidi na John Bocco na alitamani kuwa hatari kama yeye.
Salamba amekiambia kipindi cha Kabumbu na SportPesa, amesema amekuwa akivutiwa na sana na kazi nzuri ya Bocco.
“Nimekuwa nikitamani sana kuwa kama Bocco, ni mshambuliaji anayejituma na akitamani kufanya vizuri zaidi na zaidi,” alisema.
Kuhusiana na wachezaji wanaocheza soka la kulipwa, Salamba amesema, Mbwana Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji, ndiyo chaguo lake.
“Natamani kufikia alipo Samatta na ikiwezekana kuvuka. Nataka kucheza soka la kulipwa na hii ndiyo ndoto yangu,” alisema.
Salamba kwa sasa anakipiga katika kikosi cha mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Simba ambacho amejiunga nacho akitokea Lipuli FC.








Kaza tu Bro inawezekana hata kumpita Bocco, Wewe bado kinda endelea kupambambana,nguvu unazo, akili ya mpira unayo kikubwa utulivu tu,yote yanawezekana Inshallah.
ReplyDeleteJitume usichoke wala kuvunjika moyo. Subira ni chungu lakini matunda yake matamu. Climb the mountain to views the planes
ReplyDeleteSalamba yupo mahala sahihi katika wakati muafaka kama ilivyo kwa wachezaji wengi waliokuwepo Simba hasa vijana. Wanatakiwa kuichukulia Simba kama shule na wasichoke kujituma na kujifunza na kamwe wasiwe na mawazo ya kukata tamaa au kujiona wameshaufikia ustaa na kuanza kuendekeza mambo ya hovyo yaliyowakwamisha wengi kabla yao.
ReplyDelete