September 11, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Simba umesema kwa sasa hautakuwa na chochote cha kusema kuhusiana na kufungiwa kwa Meneja wa timu, Richard Robert kujihusisha na masuala ya soka mpaka pale watakapopata barua.

Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, amesema wanachosubiri hivi sasa ni barua kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili wapate mwanya wa kutoa tamko lao.

Manara ameeleza kwa sasa hana nguvu ya kueleza chochote akisema hawezi kuzungumzia taarifa za mitandaoni mpaka pale atakapopata ambazo ni rasmi.

Robert amefungiwa kujihusisha na masuala ya soka nje na ndani ya Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja baada ya kukutwa na hatia ya makosa wawili ya kuihujumu Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars na kutotii maagizo ya viongozi wa TFF na Simba.

Mbali na kifungo cha mwaka mmoja, Robert pia amepigwa faini ya shilingi za kitanzania.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic