'SIMBA INAKUFA 4-1 TAIFA LEO'
Na George Mganga
Wakati wadau na mashabiki wa mpira wa miguu nchini wakisubiria kwa hamu kipute cha mechi ya watani wa jadi katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, unaambiwa Ofisa Habari wa Yanga, ametabiri Simba kufa 4-1.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Dismas Ten ametabiri kuwa Simba itafungwa jumla ya mabao 4-1 na Yanga katika mchezo ambao utaanza majira ya saa 11 jioni.
Ten aliweka picha inayoonesha 1-4 ambapo 1 ikiwa na rangi nyekundu huku 4 ikiwa na rangi ya njano ikimaanisha kuwa Yanga itashinda mabao 4-1.
Yanga itaingia uwanjani ikiwa haina presha yoyote kufuatia kutopoteza mchezo hata mmoja huku Simba wakienda sare mmoja na kufungwa katika mechi 4 walizopiga msimu huu.
Mechi hiyo yenye msisimko wa aina yake tayari imeteka vinywa vya mashabiki kwa wiki hii nzima ambapo leo jioni itajulikana mbivu na mbichi kwa watani hao wa jadi.
Eti yanga itaingia uwanjani bila presha yoyote,wiki nzima mmejitahidi kuwajenga kisaikolojia kandambili,kwa taarifa yenu hizo NNE zinzwahusu kwani kimaandishi yanga ndiye mwenyeji hivyo anatangulia kuandikwa,hill ndio tatizo LA kuwa na wasemaji volaza,mtazidi kumpa chati manara subiri muone
ReplyDeleteUmeona safi saana
DeleteHujielew wewe unamapungufu kichwan mwako
DeleteChunga xana maneno yako! Sio lahic kama unavofikilia
ReplyDeleteChunga xana maneno yako! Sio lahic kama unavofikilia
ReplyDeleteUtatimuliwa Yanga kama wenzio waliokutangulia. Chunga domo hilo huwajui mashabiki wa Yanga wewe
ReplyDelete