September 28, 2018


Jana Alhamisi nahodha wa Yanga, Kelvin Yondani alizua taharuki baada ya kushindwa kutokea mazoezini lakini uongozi wa timu yake ukaweka mambo sawa kuwa nyota huyo ana matatizo ambayo yalimlazimu abakie hotelini.

Yondani alikosa mazoezi hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia mkoani hapa, hivyo kuzua taharuki wakati wa kuelekea mechi ya timu hiyo dhidi ya Simba, wikiendi hii. 

Taarifa zinasema kuwa baada ya kumalizika kwa mazoezi hayo ni kuwa Yondani alibaki hotelini kwa ajili ya kumaliza matatizo ya familia yake ambayo alikuwa nayo.

“Yondani ni mzima kabisa wala usihofu lolote juu yake kutokana na kutoonekana kwenye mazoezi ya leo (jana), ila fahamu kwamba hana shida yoyote ile na atakuwepo kwenye mchezo ujao dhidi ya Simba. 

“Kilichotokea kwake ni kwamba alipata tu matatizo ya kifamilia hivyo akahitaji muda wa kuyatatua ndiyo maana akabakia hotelini, lakini kesho (leo) ataungana na wenzake kwa ajili ya kuendelea na mazoezi,” alisema mmoja wa viongozi wa timu hiyo.

4 COMMENTS:

  1. Kwani Yanga ina beki mmoja tu?

    ReplyDelete
  2. Sasa lipi la kuliamini kati ya Yondani kuwa na Maleria au anamatatizo na familia yake?

    ReplyDelete
  3. Tuliocheza mpira tunaelewa 'MAMBO YA BABU'

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic