Baada ya klabu ya Mtibwa Sugar kulalamikia kutopewa fedha zake za mshindi wa Kombe la FA, Shirikisho la Soka nchini (TFF) limeibuka na kusema Mtibwa hawawezi kuzungumzia suala hilo.
Kwa mujibu wa Radio One, Mkurugenzi wa Mashindano, Salum Madadi, amesema kwa namna anavyowafahamu Mtibwa Sugar hawawezi wakatoa kauli kama hiyo.
Madadi ameeleza kuwa Mtibwa wamekuwa ni watu wastaarabu hivyo haamini kama wanaweza kuzungumza kwenye vyombo vya habari wakilalamikia kuwa hawajapewa fedha zao.
Aidha, Madadi ameeleza kuwa kwa sasa hatakuwa na kuzungumza zaidi na badala yake watakuja na tamko lao kuhusiana na fedha hizo siku za usoni.
Mtibwa inadai kitita cha fedha ambazo ni shilingi za kitanzania, milioni 50 baada ya kufanikiwa kutwaa Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Singida United Juni 2 2018 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.








Ikiwa ni hivo basi ilibidi mwafahamisha mapema kuliko kunyamaza kimya na wanapokuja kudai jawabu ni kuwa hapo zamani walikuwa wastaarabu, jee ina mana sasa wamekosa ustaarabu?
ReplyDeleteni afadhali TFF wangeaa kimya ulio uja na majibu mepesi namna hiyo kama Mtibwa wamelalamika wao walipaswa kusema pesa ziko wapi na sio bla bla hizo
DeleteJAMANI TFF SASA INAPOTOKA. BADALA YA KUTOA MAELEZO KAMA MADAI HAYO NI KWELI AMA SI KWELI WANATOA MAJIBU YASIYO NA MAANA. ELEZENI KAMA NI KWELI KWANINI KAMA SI KWELI KANUSHENI. TFF HII INAANZA KUUDHI.
ReplyDelete