TUMESIKIA KIU YENU, KAENI TAYARI KWA SPOTI XTRA JIPYA, ALHAMISI HII
Hili ni toleo la 39 tangu Gazeti hili liingie mtaani Desemba mwaka jana. Tangu siku ya kwanza tulijipambanua kwamba sisi tutawaletea kitu cha kipekee.
Tuliwaaambia kwamba tunakuja na gazeti la tofauti kabisa ambalo halifanani na magazeti yote ya michezo Tanzania. Tunashukuru kwamba mlitupokea kwa kishindo na kuzidi kutuunga mkono mpaka sasa tumekuwa gazeti imara na linalofanya vizuri zaidi miongoni mwa magazeti ya michezo Tanzania.
Tumejitofautisha na wengine kwa kuwa gazeti linalozungumza kwa takwimu zaidi kuliko maandishi. Tumejitofautisha na wengine kwa kutoa chambuzi makini zaidi pamoja na habari za kuvutia zilizoandikwa kwa ladha ya aina yake ya kiuanamichezo.
Sasa kutokana na sapoti kubwa ambayo mmeendelea kutupa pamoja na mahitaji makubwa, kiu na maombi ya wasomaji wetu kutoka sehemu mbalimbali nchini kuanzia wiki ijayo gazeti hili litakuwa likitoka mara mbili kwa wiki.
Awali lilianza kwa kutoka Jumapili tu lakini kwasasa litaanza kuingia mitaani pia siku ya Alhamisi kwa ubora mkubwa zaidi. Tumechukua maoni yenu pia kwenye mambo mbalimbali hivyo tunawahakikishia kwamba gazeti jipya la Alhamisi ambalo litaanza kuingia mtaani wiki ijayo litakuwa na ubora zaidi ya ule mliouzoea siku ya Jumapili.
Spoti Xtra inaundwa na timu makini kwenye idara mbalimbali ndio maana tunajiamini kwamba kwa sasa wasomaji mtazidi kufaidi zaidi na kupata uelewa wa mambo mengi ya kimichezo yanayojiri ndani na nje ya Tanzania.
Ujio huo wa toleo jipya utakwenda sambamba na promosheni kabambe ambayo uongozi wa Global Group umeamua kutoa kama ofa kwa wasomaji wake kulikubali gazeti hili tangu lilipoingia mitaani Desemba mwaka jana na kupindua kibabe utawala wa magazeti makongwe yaliyokuwa sokoni.
Ofa ya kwanza ambayo tumeamua kutoa kama zawadi ya mwaka kwa wasomaji wetu ni kwamba Spoti Xtra litakuwa likiuzwa kwa Sh500 tu badala ya Sh800 iliyozoweleka.
Lakini ofa nyingine ambayo inapatikana kwa wasomaji wa Spoti Xtra pekee ni kwamba tutawagawia zawadi mbalimbali za kiuanamichezo kama jezi za klabu mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Kwa kununua gazeti lako utapata namba maalumu kwenye kuponi iliyoko ndani ambayo utaelekezwa jinsi ya kutuma na kila wiki utakuwa ukishinda jezi ya klabu unayoipenda wewe. Mbali na jezi za klabu za Ulaya kuna jezi za klabu za Ligi Kuu Bara na mipira mbalimbali.
Tunaomba wasomaji wetu kama tulivyoanza pamoja na kukomaa pamoja muendelee kutupa hadhi hiyohiyo kwa kutuunga mkono katika mabadiliko mapya tunayoanza kuyafanya kuanzia wiki ijayo.
Timu ya Spoti Xtra ikiongozwa na Mhariri Mtendaji, Saleh Ally na wahariri wengine pamoja na waandishi, wachambuzi mbalimbali tunawahakikishia kwamba mambo mazuri yanakuja. Tuungeni mkono. Kumbuka toleo ya kwanza jipya la Alhamisi ni wiki ijayo Septemba 20.
0 COMMENTS:
Post a Comment