Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ameeleza kuwa Yanga wameanza vizuri kwenye ligi msimu huu na hilo litawafanya waje kwa wingi uwanjani.
Ofisa huyo mwenye maneno mengi amesema watajitahidi kuwachangia Yanga kwa sababu mapato yote ya mchezo huo yataelekea kwao wakiwa kama wenyeji wa mchezo.
Manara amefunguka hayo kutokana na klabu hiyo hivi karibuni kuanzisha mchakato wa kuchangiwa na wanachama wake ili kujikwamua na hali ngumu ambayo klabu inaipitia hivi sasa.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amesema kuwa Yanga watakuja kwa wingi kutokana na timu yao kuwa na alama 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment