September 25, 2018


Na George Mganga

Baada ya kushikwa na tumbo kisha kupelekwa hospitali akiwa kanda ya ziwa, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, jana alitembelewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Omar Kaya kwenda kumfariji.

Kaya alifunga safari kuelekea nyumbani kwa Manara ili kumjulia hali kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya tumbo lilipokelea kusumbuka kwa siku mbili mfululizo.

Baada ya Manara kupata ugeni huo alionekana kufarijika na kutoa somo dogo kwa baadhi ya wapenzi na mashabiki wa Simba na Yanga kuelewa nini maana ya utani wa jadi.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara alieleza kuwa utani wa jadi si uadui huku akifurahia namna mtani wake Kaya alivyowasili kwake na kumjulia hali.

"Sijui lini ntaeleweka ninaposema Simba na Yanga si maadui wala mahasimu, fikiria miongoni mwa watu wa mwanzo kuja kwangu kuniona baada ya kutoka hospital ni swahiba wangu ambaye ndiyo Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Omar Kaya.

"Tumeongea na kutaniana lakini pia kushauriana yenye faida kwa mpira wa Tanzania.
Mashabiki maandazi jifunzeni kwetu na kwa wachezaji, sisi hatuna uadui, msitukanane wala kukunjana, charurareni bila kugombana" aliandika.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic