September 21, 2018

Meneja wa timu ya Simba Abbas Ally amewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kutulia na kujiandaa na furaha katika mechi zijazo baada ya kufanya vibaya katika mechi mbili mfululizo. 

Abbas ametoa kauli hiyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati yao na Mbao FC uliomalizika kwa Simba kufungwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Septemba 20, 2018. 

Amesema ligi siyo mashindano ya mtoano bali ina mechi mechi nyingi hivyo atakayemaliza vizuri ndiye atakaye kuwa bingwa, na Simba bado ina nafasi hiyo. 

Kuhusu mabadiliko ya Kocha wa timu hiyo kwenye safu ya ushambuliaji, Abbas amesema kocha anapanga kikosi kulingana na jinsi wachezaji walivyofanya mazoezi na mchezaji atakayeonekana kuwa vizuri zaidi ndiye anayepewa nafasi kwenye mechi. 

Kwa upande wake beki wa Simba ambaye pia ni nahodha msaidizi wa timu hiyo Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amewataka mashabiki wa timu hiyo wasikate tamaa baada ya kufungwa na Mbao FC.

5 COMMENTS:

  1. Kabisa kunakoo malengo ya muda mrefu Simba hawana haja yakuwa na presha ni kumpa muda kocha. Timu kama Mbao wakeshakamia mechi ya Simba basi wameshamiza ligi matokeo yake wanakuja kuhangaika kupigania kutoshuka daraja.

    ReplyDelete
  2. SIMBA HAKUNA KOCHA.. FUKUZA HUYO MZUNGU HANA UWEZO WA KUFUNDISHA MPIRA LABDA MIELEKA

    ReplyDelete
  3. hamna kitu nyie simba

    ReplyDelete
  4. Hata Dylan Kerry wa Gormahia mashabiki walimpigia kelele afukuzwe pale Simba na alifukuzwa.Na kama kawaida Mungu huwa hamfichi mnafiki Mashabiki haohao waliompigia debe Kerry afukuzwe awali hivi karibuni walisikika wakimsifu Kerry na kushinikiza arejeshwe Simba. Kujenga timu yenye muunganiko wa kitimu na kuleta ushindani wa kweli kunahitaji subira na kama viongozi wa Simba watafuata mihemko ya mashabiki wake basi hakuna kocha atakaeweza kufanya kazi pale Simba.Lazima kuwe na subra kwani wachezaji hasa wazawa ambao ndio idadi kubwa ya first eleven ya Simba wanatakiwa kumpa sapoti kocha kwa kujituma zaidi kwani wamepata kocha ambae anaweza kuwasaidia kupiga hatua mbele zaidi na ndio maana timu yao inakamiwa zaidi na wachezaji wa timu nyengine ili nao wao waonekane.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic