September 21, 2018


Wakati Simba na Yanga zikitarajiwa kucheza Septemba 30, mwaka huu katika Ligi Kuu Bara, kocha mkuu wa kikosi hicho, Mbel­giji, Patrick Aussems, kwa sasa anaisaka dawa ya kuwamaliza wapinzani wake hao.

Mchezo huo ambao huwa na hisia za mashabiki wengi wa soka ndani na nje ya Tanzania, unatarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Kwa sasa Simba ipo Kanda ya Ziwa ambapo jana Al­hamisi ilitarajiwa kucheza na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba uliopo Mwanza, kabla ya wikiendi hii kupambana na Mwadui ka­tika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.

Ikitoka huko, Simba itacheza na Biashara United kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, kabla ya kuvaana na Yanga.

Simba ikiwa Kanda ya Ziwa, Aussems amesema: “Mechi hizi za huku ndizo zitatupa mwan­gaza wa nini cha kwenda kufanya katika mechi zi­jazo ukizingatia kwamba tukitoka huku tunarudi Dar na kuna mchezo mkubwa mbele yetu.

“Ni lazima tupate ushindi huku ili vijana wawe na mor­ali ya kushinda mechi zijazo za Dar.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic