September 12, 2018

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Joseph Kakunda amewaagiza wakuu wa wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri chini ya usimamizi wa wakuu wa Mikoa kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama kuwakamata watoto wote ambao huzagaa mitaani wakiomba omba pamoja na wazazi wao na washtakiwe mahakamani chini ya sheria ya elimu ya mwaka 78 inayokataza utoro. 

Naibu Waziri Kakunda ametoa maagizo hayo leo Bungeni katika mkutano wa 12 alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kiembe Samaki Zanzibar, Ibrahim Raza na kuwataka wananchi kutumia fursa zilizowekwa na serikali kwa ajili ya kujikwamua na umaskini ikiwemo Elimu bure.

Aidha Naibu Waziri Kakunda amebainisha kuwa ofisi ya mkoa wa Dar es Salaam imetekeleza hatua mbalimbali za kuwaondoa ombaomba ikiwemo kuwakamata na kuwasafirisha makwao lakini wamekuwa wakirudi.

1 COMMENTS:

  1. Hivi karibuni muheshimiwa raisi kwa maoni yake alisisitiza watanzania waendelee kuzaa bila ya kikomo kwa manufaa ya taifa imara la kesho sio wazo baya hata kidogo. Katika kumbukumbu za miaka ya hivi karibuni suala la mpango wa uzazi duniani ni kampeni iliyofanikiwa sana.lakini pia imekuwa na madhara makubwa kwa baadhi ya nchi. Nchi hasa zile zilizoendelea idadi ya watu inapungua siku hadi siku na hakuna dalili ya kuongezeka kwa hii miaka ya karibuni kiasi cha kupelekea viongozi wa mataifa hayo kupata taharuki na kuanza kutumia mabilioni ya pesa katika kufanya tafiti ya kutengeza maroboti amabayo yatakuwa na uwezo sawa na binaadamu katika shuguli mbali za jamii hata katika masuala ya mapenzi. Roboti sio mwanadamu asilani na mabillion ya pesa wanayotumia kugharamia maroboti basi zingetosha kugharamia mwanadamu katika uzazi wa kawaida na chanji ikabaki. Hata China wameiondoa sheria yao ya mtoto mmoja kwa familia. Masuala kama ya usagaji na usenge yamechangia pia kuwanya vijana wengi wa nchi zilizoendelea kutojishughisha na kuzaa na kupelekea nchi nyingi kuwa katika hatari ya kukosa nguvu kazi na kutegemea wageni. Lakini licha ya kauli ya muheshimiwa raisi kuwa watanzania waendelee kuzaa sasa kama hawa waliokwisha zaliwa wanaachiwa wakizurura hovyo kuna faida gani. Bora kuwa na mtoto mmoja mwenye faida kwenye jamii kuliko kuwa na watoto kumi wasio na faida isipokuwa sifa tu nina watoto wengi. Wahusika lazima wamsaidie kazi muheshimiwa raisi kikamilifu sio kusubiri mpaka muheshimiwa raisi kuingia barabarani kuanza kufukuzana na watoto ombaomba kwa kweli uzembe bado upo miongoni mwa watendaji wa serikali.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic