WAARABU WAMZUIA MSHAMBULIAJI STARS KUTUA DAR, ASALIA UGANDA
Kiungo mshambuliaji wa Difaa El Jadida na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Simon Msuva, juzi Jumapili alilazimika kubakia nchini Uganda baada ya klabu yake kumzuia kutokwenda jijini Dar es Salaam wakiwa na hofu ya kuchelewa kuungana na wenzake kambini mapema.
Msuva alikuwa sehemu ya kikosi cha Stars ambacho kilicheza na Uganda ‘The Cranes’ kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) na kumalizika kwa suluhu.
Kiungo huyo ambaye amekuwa na msaada mkubwa kwenye klabu yake ya Difaa, ameliambia Championi Jumatatu, kuwa alizuiwa na klabu yake kurejea Dar na wenzake wa Stars ambao waliondoka Uganda kutokana na kuhofia kwamba ratiba yake ingeingia mambo mengine wakati wanamhitaji kwa ajili ya mchezo wao wa wikiendi hii.
“Nimebaki huku Uganda na kesho (jana) asubuhi nitaondoka moja kwa moja kuelekea Morocco ikiwa ni baada ya uongozi wa klabu yangu kusema kwamba nibakie hapa ili niwahi mechi ya wiki hii.
“Walihofia kwamba naweza kwenda huko Dar kisha mambo mengine yakajitokeza na kufanya nichelewe kutua kikosini kwa wakati ambapo kuna mechi muhimu wikiendi hii,” alisema Msuva.








Safi msuva
ReplyDelete