WANACHAMA SIMBA WAIKATAA KATIBA MPYA, WAELEZA SABABU
Wakati zoezi la kurudisha fomu za wagombea nyadhifa mbalimbali katika klabu ya Simba likianza leo Jumanne, baadhi ya wanachama wameitaka katiba ya 2014 kutumika.
Wanachama hao wameeleza kuitaka katiba hiyo wakiamini ndiyo imefauata haki zote za wanasimba tofauti na mpya iliyopitishwa 2018.
Mwanachama mmoja ambaye hajataka jina lake liwekwe hadharani, amesema katiba ya 2018 ilipitishwa kiujanja ujanja kwa lengo la kuwanufaisha baadhi ya watu.
Aidha, Mwanachama huyo amefunguka kwa kusema katiba hiyo ina vipengele ambavyo vinawabana baadhi ya wanaotaka kugombea nafasi ndani ya uongozi ikiwemo suala ya kuwa na digrii badala ya elimu ya kidato cha nne.
Ukiachana na Mwanachama huyo aliyepinga, wanachama wengine wameonesha kuiunga mkono katiba mpya ambayo ndiyo itatumika kwa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Novemba 3 2018.
Wanachama hao wameeleza katiba hiyo itawafungulia milango mizuri kuelekea mfumo wa muundo mpya ambao Simba inaelekea kuuanza rasmi ikiwa chini ya Mwekezaji.








Aliyetoa maoni hapo ni mwanachama mmoja kichwa cha habari cha uchochezi mtupu.Basi limeshaondoka stendi. Latina inayotumika ni ya 2018.Hatutaki vihiyo kwenye uongozi wa juu.Vile vile hatutaki makanjanja kwenye uandishi wa habari.Tunahitaji waandishi wasomi wenye maono ya kuleta maendeleo na kuhoji kisomi sio wapika majungu nä wachochezi utafikiri sio blogu au gazeti la maana bali vigenge vya kahawa.
ReplyDeleteHaki ya Mungu tunaipenda na yuna imani kubwa na timu na viongozi wake na tunaimani na katiba mpya na kwa pamoja tuiunge mkono sio wakati wa kulaumiana mambo yende shuari kama ilivo na hiyo ndio sifa ya Simba inayoongoza kwa mapenzi
ReplyDeleteKwani kuna MTU kakatazwa kuwa na degree,wakasome ili wagombee
ReplyDeleteMe naona hata waandishi wetu ni changamoto anamuhoji mwanachama kwa interest zake.Natamani nifahamu kiwango cha elimu cha Huyo mwandishi.Haiwezekani unaenda kuhoji watu ambao wao wenyewe ndio walioipitisha katiba bila pingamizi halafu Leo unakuja kusema hawaitaki.Huwezi kuingia kwenye mabadiliko ya uendeshaji wa kisasa halafu uwatumie watu wenye upeo mdogo kwenye uongozi.Kwa ukubwa wa vilabu vyetu sio mda wa kuongozwa na watu wa form four. Hao wanapinga watu wenye digrii nao wakasome digrii kaatiba mpya haijawanyima watu kwenda kusoma.Tena muishuru Mungu katiba inawahitaji wasomi maana take inawaambia wanachama mkaome.Yaani mo aje kumwaga hela kwa uongozi usio na mpango mkakati wa maendeleo? Sahau
ReplyDelete