BAADA YA KUMTWANGA EGGINGTON, MWAKINYO AMTAKA BONDIA HUYU MKUBWA MAREKANI
Ikiwa ni saa chache baada ya Bondia kutoka Tanzania, Hassan Mwakinyo (23), kumtwanga Bondia wa Uingereza, Sam Eggington (25) katika raundi ya pili kwa TKO, ametangaza nia ya kutaka kupambana na bondia maarufu kutoka Uingereza Amir Khan.
Pambano la Jumamosi la Mwakinyo na Eggington lilikuwa la uzito wa kati lilikuwa la utangulizi kabla ya pambano kubwa la Amir Khan dhidi ya Samuel Vargas. Khan alishinda kwa tofauti ya alama dhidi ya Vargas.
Mwakinyo aliingia katika uga wa Arena Birmingham, jijini Birmingham Uingereza kama mbadala wa bondia mengine aliyetakiwa kupambana na Eggington kushindwa kufikia vigezo. Wachambuzi wengi wa masuala ya masumbwi waliliona pambano hilo kuwa rahisi kwa Eggignton ambaye alikuwa na rekodi bora zaidi lakini mambo yalimbadilikia.
Mara baada ya ushindi huo, Mwakinyo alisikika akiimba kuwa anata kupambana na bondia mwengine kutoka Uingereza, Kell Brook.
“Yeye (Eggington) aliingia ulingoni akiwa mwenye kujiamini sana. Nilitaka kuonesha uwezo wangu, sie wengine ni mabingwa pia lakini hatuonekani kutokana na mzingira tunayoishi, nimefurahi sana kwa ushindi huu na nimeionesha dunia uwezo wangu halisi,” alisema Mwakinyo baada ya pambano hilo.
“Sasa nataka kupambana na Kell Brook, na na nikishamchapa namtaka Amir Khan,” alipoulizwa kama wataweza kustahmili nguvu za Brook akajibu kwa kujiamini: “Kwani wanionaje?”








0 COMMENTS:
Post a Comment