WAWILI WA KIMATAIFA KUONGEZA NGUVU SIMBA
Wachezaji wa kimataifa wa Simba wanatarajiwa kuripoti kambini leo Jumatano kwa ajili ya kuungana na wenzao kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda.
Wachezaji ambao wanatarajia kuungana na kikosi kesho ni pamoja na Meddie Kagere, Haruna Niyonzima, Clayotus Chama na Emmanuel Okwi wachezaji hao walikuwa kwenye majukumu ya timu zao za taifa.
Simba wataondoka Dar kesho Alhamisi kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Ndanda ambao utapigwa katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Kocha wa timu hiyo, Mbelgiji Patrick Aussems alisema wachezaji hao wataungana kwa ajili ya kuendelea na maandalizi ya mchezo ujao wa ligi kuu.
“Wachezaji wetu wanarejea baada ya kumaliza majukumu yao kwenye timu za taifa hadi Jumatano (leo) wanatakiwa kuungana na wenzao kuanza mazoezi mpaka sasa mchezaji ambaye amewasili ni Aishi Manula na ameanza mazoezi.
“Wote wanatakiwa kuwa hapa ili kuweza kuwa sawa na programu zetu bila tatizo lolote kama,”alisema kocha huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment