YANGA YAWASIFIA WACHEZAJI WAKE KUWA NA NIDHAMU, YAFUNGUKA KUHUSIANA NA MAJERUHI
Mabosi wa klabu ya Yanga wamesema kuwa wachezaji wao wote waliokuwa kwenye kikosi cha Taifa Stars tayari wamesharejea kambini.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili kupitia Radio One, Hussein Nyika, amesema Yanga imebahatika kuwa na wachezaji wenye nidhamu ambao wameripoti kambini kwa wakati.
Wakati kikosi kikijiandaa kuelekea mechi na Stand United, Nyika ameeleza kuwa hakuna mchezaji ambaye ni majeruhi mpaka sasa.
Nyika ameeleza kuwa mchezaji pekee aliyekuwa majeruhi, Kelvin Yondani, tayari ameshaanza mazoezi mepesi na wenzake.
Kikosi hicho kitashuka dimbani wiki hii kukipiga na Stand United ya Shinyanga ambao inaelezwa tayari wameshawasili jijini hapa.
Hiyo migomo ya kila mara ndio nidhamu?
ReplyDeleteWalikikuwa wakigoma sababu ya madai yao ya mishahara sio kwa kukosa nidhamu
ReplyDeleteTafsiri ya nidhamu ni kufuata utaratibu katika kutenda jambo. Kugoma kwasababu yoyote ile ni ukosefu wa nidhamu.
Delete