September 23, 2018


Na George Mganga

Dakika 90 zimemalizika kutoka Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya SIngida United.

Mabao yote mawili yamewekwa kimiani na mshambuliaji Mrundi, Amis Tambwe katika dakika za 30 na 45+.

Matokeo hayo yanazidi kuiweka Yanga juu ya kilele cha msimamo wa ligi ikifiksha alama 12 nakuwaacha watani zao wa jadi Simba walio na alama 10.

Katika mchezo huo Mfadhili wa klabu ya Singida United, Mwigulu Lameck Nchemba alikuwa jukwaani kushuhudia timu yake ikiangukia pua kwa mara pili mfululizo baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya African Lyon.

Baada ya kibarua cha leo Yanga sasa itaanza maandalizi kujiwinda na watani zao wa jadi Simba kuelekea mchezo utakaopigwa Septemba 30 2018.

5 COMMENTS:

  1. Hii timu ya singida mbona msimu huu naiyona si kama ile ya msimu uliopita kuna mini?

    ReplyDelete
  2. hongeren watan,ila inshu itakuwa mikoani

    ReplyDelete
  3. Jamani wandishi wetu, uraia mtu kutoka Burundi sio mburundi ni mrundi. Na kutoka Rwanda sio mrwanda ni myarwanda. Huwezi kusema eti goli limefungwa na mburundi Amis Tambwe, bali goli limefungwa na mrudi Amis Tabwe. Pia, huwezi kusema limefungwa na mrwanda Haruna Niyonzima, bali Goli limefungwa na mnyarwanda Haruna Niyonzima. Mnaudhi kwasababu mnaweza kudhani kuwa mnajua na mnafanya kusudi, lakini mnawapotosha watoto wetu hasa ambao bado wanajifunza uraia wa watu kutoka mataifa mbalimbali. Shame on you!

    ReplyDelete
    Replies
    1. kwan ameaandika mburundi? au ww hujasoma bali umekoment tu?"Mabao yote mawili yamewekwa kimiani na mshambuliaji Mrundi, Amis Tambwe katika dakika za 30 na 45+".

      Delete
  4. Yanga kuifunga Singida sawa na mtu kumtafuna hawara wake kuna jambo gani jimpya? Singida ni shamba la bibi la Yanga na sio singida kuipa yanga mabao na points Singida pia huigaia Yanga wachezaji bure. Kwa hivyo hakuna mzigo wowote Yanga inayoipa Simba na wao wenyewe yanga wanajua. Mwigulu Mchemba hawezi kukubali Singida iifunge yanga wakati wakielekea kucheza na Simba. Singida haiwezi kukaa na itaeseka sana kwa kuundekeza uyanga usiokuwa na manufaa yeyote kwenye klabu yao.kama Toto Africans ilivyofulia na singida nao wanaelekea hukohuko.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic