September 24, 2018


Mashabiki wa soka duniani walisherehekea mwezi huu wa Septemba, mwaka huu miaka 18 ya kung’ara kwa miongoni mwa mastraika hatari duniani, Lionel Messi, ambaye jina la utani ni `La Pulga’.

Messi alitinga kwenye medani ya soka Septemba 17, mwaka 2000, akiwa na umri wa miaka 13, ambapo alitoka kwao Rosario, Argentina na kujiunga na kituo cha kulelea yosso cha La Masia kinachomilikiwa na Barcelona.

Staa huyo aliibukia katika timu ya watoto wa Newell’s Old Boys ya Argentina, ambako mawakala wa Barcelona ndio walimwona.

Kufikia mwaka 2018, Messi sasa ni jina kubwa katika soka na anahesabiwa kama miongoni mwa wanasoka hatari kuwahi kutokea duniani.

Messi amepachika mabao 570 katika mechi 675, ambapo pia ametoa asisti 215.

Pia tangu ameanza kucheza soka amefanikiwa kushinda mataji 33 ya mashindano mbalimbali ya soka.

Messi ni mchezaji mwenye mafanikio makubwa zaidi katika kikosi cha sasa cha Barcelona.

Amet-euliwa mara tano kuwa Mwanasoka Bora was dunia na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).


taa wa zamani wa Barcelona, Xavi Hernandez aliwahi kueleza jinsi walivyokuwa wanashangazwa na kipaji cha hali ya juu cha Messi.
Xavi alisema kuwa katika siku za mwanzo, Messi alikuwa anawatesa sana katika mazoezi ya Barcelona wakongwe kama akina Lilian Thuram.

MAMBO USIYOYAJUA KUHUSU MESSI
  1. MSHAMBULIAJI MFUPI ZAIDI DUNIANI
Messi ana urefu wa mita1.69, ambao unamfanya awe straika mfupi zaidi duniani ingawa pamoja na umbo hilo bado hakamatiki likija suala la kupiga mabao.

  1. MCHEZAJI MDOGO ZAIDI KUWANIA TUZO YA MWANA-SOKA BORA WA DUNIA
Akiwa na umri wa miaka 21, aliteuliwa mwaka 2008 kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, ambayo ilikuwa rekodi kwa mchezaji mdogo kuwania tuzo hiyo.

  1. MCHEZAJI WA KWANZA KUWA MWANASOKA BORA WA DUNIA KWA MIAKA 4 MFULULIZO.
Messi ameweka rekodi ya mwanasoka wa kwanza kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa dunia mara nne mfululizo.

  1. TATIZO LA KUKOSA HOMONI ZA KUKUA
Messi aligundulika na tatizo la kukosa homoni za kukua. Tatizo kubwa ni wazazi wake walikuwa hawana ubavu wa kulipa matibabu ya mchezaji huyo.

  1. REKODI YA BARCELONA KUFUNGA `HAT-TRICK’ NYINGI
Messi ndio anashikilia rekodi ya kufunga `hat-trick’ nyingi zaidi katika kikosi cha Barcelona.

  1. MFUN-GAJI BORA ULAYA
Messi ana rekodi ya kuwa mfungaji bora wa ligi za Ulaya mara tatu.

  1. MKA-TABA WAKE WA KWANZA ULISAI-NIWA KWENYE KITAMBAA CHA MEZANI
Barcelona ilikuwa inahofia kumkosa mchezaji huyo lakini maofisa wake walikwenda bila ya karatasi walipokwenda kukutana nao. Wakatumia kitambaa kusaini makubaliano.

  1. MESSI ANAPENDA SANA MSOSI
Messi anasifika kwa kupenda kula. Uongozi wa Barcelona ulilazimika kuanzisha utaratibu wa kuweka vyakula vya aina mbalimbali kwa sababu ya Messi.

  1. MTOTO WA MESSI ASAJILIWA AKIWA NA SIKU TATU ZA KUZALIWA
Mtoto wa kwanza wa Messi anayeitwa Thiago anatazamiwa kujiunga na Newell’s Old Boys.
Katika hali ya kushangaza alisainiwa mkataba akiwa na siku tatu tangu kuzaliwa.

  1. MESSI ALIFAHAMIANA NA MKEWE AKIWA NA MIAKA MITANO
Messi alifahamiana na mkewe akiwa na umri wa miaka mitano kutokana na familia zao kuwa marafiki.

  1. MESSI NI BALOZI WA WATOTO
Messi ni Balozi wa Shirika la Umoja la Mataifa la Kushughulikia Masuala ya Watoto (UNICEF).

  1. REKODI YA KUFUNGA MABAO MENGI KATIKA MWAKA
Messi aliweka rekodi ya dunia ya kufunga mabao mengi katika mwaka baada ya kupachika mabao 91 mwaka 2012.

  1. KUFUNGA MARA 14 UEFA
Messi pia anashikilia rekodi ya kufunga mashindano 14 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic