October 8, 2018


Akifunga bao lake la kwanza katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara, kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya ameibuka na kutamba kuwa huo ni mwanzo, bado ataendelea kufumania nyavu.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni saa chache tangu mchezo wao wa saba wa ligi umalizike dhidi ya African Lyon uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Sa­laam na matokeo kumalizika kwa ushindi wa mabao 2-1 yakifun­gwa na Emmanuel Okwi na yeye mwenyewe Kichuya.

Matokeo hayo yanaifanya Simba iwe katika nafasi ya nane ikiwa na pointi 13 ikicheza michezo saba ya ligi katika msimu huu huku Mtibwa Sugar ikiongoza ikivuna pointi 16, wakicheza mechi nane.

Kichuya alisema hakuna mchezaji asiyependa kufunga lakini majukumu ambayo amepewa na kocha wake Mbelgiji, Patrick Aussems ndiyo yamefanya ashindwe kufunga.



Kichuya alisema, bao hilo alilolif­unga ni mwanzo wake mzuri kwa yeye kuendelea kufunga katika michezo ijayo ya ligi huku akishiri­kiana na wenzake katika kuipa mafanikio timu yao.

Aliongeza kuwa, hakuna kitaka­choshindikana kwake, kikubwa amepanga kutumia vema kila nafa­si atakayoipata kwa ajili ya kufunga mabao huku akitimiza jukumu lake jingine la kutengeneza mabao.

“Katika timu yetu kila mche­zaji ana majukumu yake ambayo amepewa na kocha ambayo ni lazima kila mmoja ayafanye kwa usahihi katika kuhakikisha timu inapata matokeo mazuri.

“Mimi binafsi nina majukumu ambayo nimepewa na kocha ambayo nisingependa kuyaweka wazi lakini kwa kifupi niseme kuwa mimi jukumu langu ni kuwaten­genezea washambuliaji nafasi za kufunga mabao.

“Lakini kama ikitokea nikipata nafasi nzuri ya kufunga kama niliy­oipata katika mechi na Lyon, basi nitaitumia vema kufunga mabao na huo ndiyo mwanzo wangu mzuri katika msimu huu wa ligi,” alisema Kichuya. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic