KIUNGO YANGA AISHIKA VIZURI TIMU
Kiungo mshambuliaji anayeongoza kwa asisti nyingi Yanga, Ibrahim Ajibu, ameibuka na kuwaambia maneno mazuri ya kuwatia matumaini mashabiki wa timu hiyo, kwa kutamka kuwa mashabiki wasihofu, mambo mazuri yanakuja.
Kauli hiyo aliitoa ikiwa ni saa chache kabla ya pambano lao dhidi ya Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara jana Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Championi Jumatatu, Ajibu alisema wao kama wachezaji wanatambua umuhimu wa mashabiki wao, hivyo ni lazima wapate matokeo mazuri katika michezo ijayo ya ligi ili kuhakikisha wanafanikisha malengo yao.
Ajibu alisema, wanafahamu ugumu wa ligi uliopo katika msimu huu, lakini watahakikisha wanafanya kila liwezekanalo kufanikisha ushindi huku akiwataka mashabiki kutokata tamaa kujitokeza uwanjani, pale wanapopata matokeo mabaya.
“Tunataka kuona timu yetu ikiendelea kupata matokeo mazuri,” alisema Ajibu.
Kwa mechi za nyumbani mnajisifu,ngojeni muone ugenini kama mtakohoa,mpira ndivyo ulivyo,labda muendelee kubebwa kama kawaida yenu hii tff imeoza,okwi amekatwa kwenye box tena karibu na goli lakini refa kapeta,coast nao wamefanyiwa hivyo hivyo mechi na azam ila chamsingi ni kuzoea tu kwamba Tanzania mwenye mpira ni yanga pekee labda na hao azam,wasimamiz wa ligi kama hawaoni yanayofanyika.
ReplyDelete