October 27, 2018


Kocha Mkuu wa timu ya Azam, Hans Pluijm amesema kuwa hana mashaka na uwezo wa wachezaji wake haoni kikosi ambacho kitamsumbua kwa sasa.

Pluijm amefanikiwa kuingoza timu yake kucheza michezo 10 bila kupoteza, amepata sare tatu na kushinda michezo saba amejikusanyia pointi 24 na kushika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

"Vijana wangu wana uwezo wa mzuri na wananishangaza hasa uwanjani, nawaona wakifanya makubwa na wataleta ushindani kwa michezo yote ya ligi kuu iwe nyumbani ama ugenini tutapata matokeo.

"Simba na Yanga ni timu ambazo zina majina makubwa ila siliangalii ninachojua nimejipanga kushindana na timu zote kwenye ligi na wachezaji wangu nimewaambia ninataka matokeo, kazi bado inaendelea tutafanya makubwa msimu huu," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic