Taarifa zilizotufikia alfajiri ya leo, Oktoba 20, 2018, zinasema kuwa Mfanyabiashara Bilionea Mohamed Dewji maarufu kwa jina la Mo Dewji amepatikana baada ya kutupwa eneo la Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Mo Deji amerejea nyumbani kwake kuungana na familia yake akiwa salama baada ya kupatikana usiku wa kuamkia leo kutokana na watekaji hao kumuachia wakitumia gari lilelile walilotumia kumteka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Dar es Salaam, Mambosasa amesema Mo amerejea nyumba ikiwa ni siku ya tisa baada ya kutekwa na watu wasiojulikana Alhamis Oktoba 11 katika Hoteli ya Colessium iliyopo Masaki jijini Dar es salaam.
"Watekaji wamemuachia, Mo yuko salama," alisema Mambosasa.
Akitoa taarifa hizo kuptia mtandao wa Twitter unaomilikiwa na Kampuni yake ya Mohamed Enterprises Ltd, Mo ameandika: “Namshukuru Mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani. Nawashukuru Watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao. Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo Jeshi la Polisi, zilizofanya kazi ya kuhakikisha narudi salama.” — Mohammed Dewji na , taarifa ambayo aliipost Saa 9:15 alfajiri, saa za Tanzania.
Aidha, Waziri wa Mazingira, Januari Makamba, nae kupitia mtandao wake wa Twitter, amethibitisha kupatikana kwa Mo na kusema kuwa Mfanyabiashara huyo alitupwa maeneo ya Gymkhana huku akiwa na alama za kufungwa kamba mikononi.
“Nimemuona na kuongea kwa kirefu na Mohammed Dewji. Ni mzima wa afya isipokuwa ana alama za kufungwa kamba mikononi na miguuni. Mnamo saa nane usiku, watekaji waliamua kumtupa kwenye maeneo ya viwanja vya Gymkana. Naamini Polisi watatoa taarifa za ziada kuhusu kilichojiri,” ameandika Makamba.
Hii ndio tanzania, haya tusiongee sana ahsante ccm.
ReplyDeleteIla kijana bado sana,upo nyuma sana,suala la mo kupatikana limethibitika tangu saa nane za usiku iweje unatuambia ni breaking news?pole sana kijana ongeza juhudi.
ReplyDeleteIla kijana bado sana,upo nyuma sana,suala la mo kupatikana limethibitika tangu saa nane za usiku iweje unatuambia ni breaking news?pole sana kijana ongeza juhudi.
ReplyDelete