JESHI LA POLISI LATOA TAMKO JINGINE KUHUSIANA NA MO DEWJI
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati juhudi kubwa zikifanyika kuhakikisha bilionea kijana Tanzania na Afrika, Mohammed Dewji 'Mo' anapatikana.
Hatua hiyo imekuja kutokana na uchunguzi ambao jeshi hilo linazidi kuufanya tangu kutekwa kwa Dewji siku ya jana wakati akielekea kufanya mazoezi maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam.
Dewji alitekwa na watu ambao bado hawajatambulika na kupiga risasi hewani ili kutishia watu kisha kwenda naye pasikojulikana.
Jeshi limezidi kuwataka wananchi kuwa na subira kwani uchunguzi unazidi kufanyika usiku na mchana kuhakikisha Mo anapatikana.
0 COMMENTS:
Post a Comment