KAKOLANYA AFICHUA SIRI YA MAFANIKIO
Mlinda mlango wa timu ya Yanga ambaye mashabiki wa Simba bado hawajamsahau, Beno Kakolanya amefichua siri ya mafanikio baada ya kuweza kucheza michezo minne bila kuruhusu bao katika mechi dhidi ya Simba,Singida United,Mbao FC na Alliance.
Kakolanya amesema kikubwa kinachomsaidia kuwa katika ubora ni kujiamini katika kazi yake anayoifanya pamoja na maelewano mazuri ya safu ya ulinzi.
"Jambo la kumshukuru Mungu kwa kuweza kufikia mafanikio haya,lengo langu ni kuweza kuendeleza rekodi hii katika michezo mingine inayofuata.
"Maelewano yaliyopo kwa safu ya ulinzi yanasaidia kuwa katika ubora ambao nipo nao, ninazidisha umakini kila ninapokuwa uwanjani ili kufanikiwa "alisema .
0 COMMENTS:
Post a Comment