October 20, 2018


Baada ya kupatikana muwekezaji wa timu ya Simba Mohamed Dewj "Mo" habari kutoka ndani ya Simba zimeeleza kuwa kesho atakuwepo uwanja wa taifa kushuhudia mchezo wa Simba na Stand United.

Simba atacheza kesho na Stand United huku wachezaji na wapenzi wa Simba wakiwa na furaha kubwa kutokana na kuonekana kwa muwekezaji huyo ambaye ni bilionea kijana mpenda michezo.

 Mo Dewji amepatikana ikiwa ni siku 9 baada ya kutekwa na watu wasiojulikana October 11, katika Hotel ya Colessium iliyopo Masaki, ameungana na familia yake akiwa salama baada ya kupatikana usiku wa kuamkia leo kutokana na watekaji hao kumuachia wakitumia gari lilelile walilotumia kumteka.


5 COMMENTS:

  1. Ila polisi na serikali wana kila sababu za kukemea tabia za wanasiasa wetu hasa wale wa upizani jinsi wanavyojitahidi kuupotosha umma na kubeza kazi kubwa inayofanywa na jeshi letu la polisi. Mwanzoni mapema mwa utekaji wa Mo nilipitia nakala kadhaa za vyombo vya habari vya nje kutaka kujua vinasemaje juu ya tukio lile kutokea hapa nchini vyombo vya habari kama vile Reuters,BBC,CNN nakadhalika. Nichogundua hata wao walishangazwa na jambo kama lile kutokea Daresalam. Walizungumzia majiji kadhaa ya Africa ambayo vitu kama vile vya utekaji vingeweza kutokea lakini sio Daresalam . Waliuliza how safe is Daresalam? na jibu likawa it is very safe when you compare to other African big cities.lakini utaona watanzania wanasiasa wetu wanavyolazimisha kuuaminisha ulimwengu kuwa Daresalam sio mji salama na hata kudiriki kufika mbali kujaribu kuihusisha serikali kuwa inahusika na matokeo hayo ya utekaji. Katika tukio hili la Mo nadhani watanzania itakuwa tumejifunza mengi na kubwa zaidi jeshi letu la polisi ni chombo kinachopaswa kuheshimiwa katika utendaji wa kazi yake na wana stahiki kupewa ushirikiano zaidi kuliko kushushiwa tuhuma za kipumbavu.

    ReplyDelete
  2. Hii itakua ni tiba ya kisaikolojia kwa wachezaji, wapenzi, viongozi na wanachama wa simba

    ReplyDelete
  3. Kwa kweli kwa kiasi fulani kuna baadhi ya wanasiasa wana matatizo. Mfano vyombo vya usalama nchini vimeweka wazi yakuwa walimfahamu mmiliki wa gari lilohusika na uhalifu katika utekaji wa Mo kupitia Interpol yaani international police ndio waliowapa taarifa kamailiki za lile gari pengine hata picha zile mubashara za lile gari ni kazi ya Interpol lakini bado kuna hawa watu sijui tuwaite wanasiasa au maadui wa nchi yetu waliendelea kusema eti usalama wa Taifa huwa wanatumia plate namba za nje wakimaanisha kuwa lile gari ni la usalama wa taifa Jamani? Kwa kweli naona Serikali na vyombo vyake vya usalama nimekuwa na subira za hawa watu lakini utaona kabisa mtu Lema..anailazimisha mamlaka kumchukia hatua lakini Serikali inamuangalia tu alafu naendelea na porojo zake kuwa nchi haina uhuru mtu wa mtu kujieza nakadhalika nakadhalika.kwa bahati nimesha tembelea nchi kadhaa Duniani na ni tanzania pekee ambapo baadhi ya raia wake wanalichafua jeshi lao la polisi kwa madhumuni ya kuliondelea imani kwa jamii halafu hawaichukiliwi hatua yeyote. Ukifuatilia matokeo ya kipolisi na raia nchi kama Marekani basi ungetarajia kuona wanasiasa hasa wale wa upinzani wakiendesha kampeni za kisiasa zidi ya polisi,lakini kamwe huwezi kukiona kitu kama hicho. Labda unaweza kuwaona wanaharakari wa haki za kijamii lakini haingii akilini muwakilishi wa wananchi bungeni anakuwa mtu wa mstari mbele wa kulipiga vita jeshi la polisi kwa kueneza uongo? Hivyo ni vitu vya hatari sana kwa mwanasiasa kuongoza kujenga uadui kati ya wananchi na jeshi lao la polisi ni vitu vya hatari sana na tungeomba wahusika kuaacha tabia hiyo mara moja kwa manufaa ya nchi yetu na usalama wake.

    ReplyDelete
  4. Mimi ninaomba sana polisi wawakamate hawa watekaji na najua watashika kama hawajawashika tayari halafu tuone hawa wanasiasa wanaoeneza uongo zidi ya serikali na jeshi la polisi watasemaje? Labda watasema wametumwa na serikali ya ccm kutoka huko walikotoka kuja kufanya uhalifu nchini?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic